Elfu 19 wafariki kwenye tetemeko

0
332

Idadi ya watu waliofariki dunia katika tetemeko la ardhi kwenye nchi za Uturuki na Syria imefikia zaidi ya elfu 19.

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema nchi yake imepata madhara makubwa kutokana na tetemeko hilo ikiwa ni pamoja na vifo vingi na uharibifu wa mali.

Habari zaidi kutoka katika mataifa hayo zinaeleza kuwa, matumaini ya kuwapata watu wakiwa hai ambao inasemekana bado wamenasa katika vifusi yanazidi kupungua ikiwa ni saa 72 tangu kutokea kwa tetemeko hilo.

Waokoaji wanaoendelea na kazi ya uokoaji wanasema kuwa, huenda idadi ya watu waliofariki dunia ikaongezeka.