Dunia yafikisha watu bilioni nane

0
140

Dunia imetimiza watu bilioni nane kwa mara ya kwanza leo Novemba 15, 2022, na hii imechukua miaka 12 kufikia idadi hiyo.

Inakadiriwa baada ya miaka 12 ijayo dunia itakuwa na watu bilioni tisa ingawa kwa sasa dunia inakumbana na mabadiliko ya tabianchi na mabilioni ya watu wanaishi katika mazingira magumu, mamia ya mamilioni wanakabiliwa na utapiamlo pamoja na njaa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia vyombo vya habari amesema

“Iwapo hatutaziba pengo lililopo kati ya matajiri na maskini, tutajitia hatiani wenyewe kuishi katika ulimwengu wa watu bilioni nane ulioghubikwa na mivutano na kutoaminiana, migogoro na vita.”

Watu katika nchi tajiri zaidi wanaweza kuishi hadi miaka 30 zaidi kuliko watu katika nchi maskini zaidi.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa ustawi wa idadi ya watu duniani kwa ujumla unavyoongezeka na matokeo ya afya yanaboreka, ukosefu wa usawa nao unaongezeka.