Mgonjwa wa mwisho aliyekuwa akiugua ugonjwa wa Ebola na kulazwa hospitalini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), ameruhusiwa na kufanya nchi hiyo kutokuwa na mgonjwa hata mmoja wa Ebola.
Ndugu wa mgonjwa huyo, yeye mwenyewe na wafanyakazi wa idara ya afya katika hospitali aliyokuwa amelazwa wameonekana wakicheza na kufurahia tukio la mgonjwa huyo kuruhusiwa akiwa na afya njema.
Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) likishirikiana na madaktari wa kimataifa waliokuwa wakihudumia wagonjwa wa Ebola huko DRC watalazimika kusubiri kwa muda wa siku 28, ili hatimaye kutangaza rasmi kuwa nchi hiyo haina Ebola.
Maelfu ya watu wamekufa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya Ebola kuikumba Jamhuri hiyo miaka minne iliyopita.