Dkt. Ndumbaro ateta na Kamishna wa Haki za Binadamu UN

0
174

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amefanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN)Michelle Bachelet kwa ajili ya kubadilishana mawazo juu ya masuala ya haki za binadamu ikiwemo kutolea ufafanuzi tuhuma kuhusu Pori Tengefu la Loliondo na Hifadhi ya  Ngorongoro.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za umoja wa mataifa za Geneva Uswisi.

Kwa upande wake, Bachelet ameshukuru na kupongeza serikali ya Tanzania kwa namna ambavyo inatekeleza masuala ya haki za binadamu

Katika mkutano huo Dkt. Ndumbaro ameambatana na Maimuna Tarishi, Balozi wa Tanzania Nchini Uswisi na Balozi Hoyce Temu ambaye ni Balozi Msaidizi wa Tanzania katika Ofisi za umoja wa mataifa, Mjini Geneva.