Dkt. Mwinyi kushiriki Jukwaa la kimataifa la uchumi

0
300

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi yupo Doha, Qatar
kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la Tatu la Uchumi.

Jukwaa hilo linalodhaminiwa na kampuni ya Kimataifa ya Bloomberg, lina kauli mbiu inayosema “Simulizi za Ukuaji Kimataifa“, na hufanyika Qatar kila mwaka.

Maelfu ya washiriki wanatarajiwa kuhudhuria Jukwaa hilo wakiwemo viongozi wa kampuni kubwa
duniani na viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali mbalimbali.