Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 21 la Doha (Doha Forum) akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pamoja na mambo mengine, baada ya ufunguzi jukwaa hilo limejadili mzozo wa Mashariki ya Kati baina ya Israel na Palestina, kwa kuangazia nini kifanyike kuutatua.