Defao azikwa kitaifa DRC

0
297

Mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo François Lulendo Matumona, maarufu General Defao amezikwa Jumamosi hii katika mazishi ya kitaifa.

Defao alifariki mwezi Desemba mwaka jana katika hospitali Laquintinie huko Douala, Cameroon, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Ndugu na jamaa zake wanasema mwanamuziki huyu hakuacha mtoto.

Wanamuziki wenzake na mashabiki wake waliohudhuri mazishi hayo wakiwa wamevalia mavazi za bei ghali wakidai pia Defao alikuwa mmoja wao, na wanafanya maonesho ya mavazi.