Dawa mpya ya upara yaidhinishwa

0
161

Kwa nchi za bara Afrika hali ya kuwa na Upara inachukuliwa si suala muhimu sana, lakini kwa kwa mabara mengine ni suala muhimu kiafya pamoja na kimuonekano.

Kwa kudhihirisha umuhimu wa suala hilo huko nchini.Marekani
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya nchini humo (FDA) imeidhinisha dawa mpya yenye uwezo wa kutibu hali hiyo inayoitwa Olumiant (baricitinib) iliyotengenezwa na kampuni ya dawa ya Eli Lilly ya nchini humo.

Mtu mwenye hali ya upara anatakiwa kuweza dawa hiyo mara moja kwa siku ikiwa ni matibabu ya awali, na.dawa hiyo ya kumeza inaweza ikawa ni.ya kwanza kwa ajili ya matibabu ya hali hiyo.

FDA imeidhinisha dawa hiyo ya Olumiant (baricitinib) kuwa ya matibabu ya hali ya upara baada ya kupatikana kwa mafanikio makubwa kufuatia majaribio yaliyofanyika.

Katika jaribio la kwanza kulikuwa na washiriki184 ambao kila mmoja alipewa gramu 2 za Olumiant, 281 walipewa gramu 5 ambapo matokeo yameonesha asilimia 22 ya waliopewa gramu 2 na asilimia 35 ya waliopewa gramu 4 walipata chanjo ya kutosha ya nywele za kichwa.

Katika jaribio la pili, washiriki 156 walipatiwa gramu 2 na 234 gramu 4 ambapo ,matokeo yalikuwa sawa na jaribio la kwanza kwa asilimia 17 ya wale waliopatiwa gramu 2 na asilimia 32 ya wale waliopatiwa gramu 4 walipata chanjo ya kutosha ya kichwa .

Una maoni gani?