China yatangaza kutokua na maambukizi mapya ya corona

0
696

Serikali ya China imetangaza kuwa kwa mara ya kwanza kwa siku ya leo hakuna hata mtu mmoja aliyepata maambukizi mapya ya virusi vya corona, hali inayofanya kasi ya ugonjwa huo ulioanzia nchini humo kuendelea kupungua.

Kupungua kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini China kumeleta faraja kwa wataalamu wa afya, ambao wamesema hatimaye juhudi zao kubwa za muda mrefu zimezaa matunda na matumaini mapya yamenza kujitokeza.

Baadhi ya raia wa China waliokuwa nje ya nchi ambao walikuwa wamezuiwa kuingia nchini humo kwa hofu ya virusi vya corona wameanza kurejea nyumbani, wakiwa na ari mpya ya kufufua uchumi wa Taifa hilo uliokuwa umetikiswa kutokana na mlipuko wa corona.