China yatanda hofu juu ya maambukizi mapya ya Corona

0
450

Mji wa Jilin, China umejawa hofu na wasiwasi wa mlipoko wa maambukizi mapya ya virusi vya Corona kwa wakazi wa mji huo.

Uongozi wa mji wa Jilin umesema, kumekuwa na maambukizi mapya vya virusi vya Corona kwenye mji huo, na ambayo yanaonekana kusambaa kwa kasi, na kutishia usalama wa wananchi.

Mlipuko wa virusi vya Corona ulianzia katika mji wa Wuhan nchini humo na kisha kusambaa katika maeneo mengine na hatimaye kuathiri nchi zaidi ya 200 duniani.