Nchi za Urusi na China zimesusia kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kinachojadili tuhuma za matumizi ya kemikali za sumu katika vita inayoendelea nchini Syria.
Nchi nyingine iliyosusia kikao hicho ambacho kinaendeshwa kwa njia ya video kwa satelite ni nchi mwenyeji ya Syria, ambakoo inatuhumiwa kuwa silaha hizo zilitumika na serikali ya nchi hiyo dhidi ya waasi.
Urusi imesema sababu kubwa ya nchi hiyo kususia kikao hicho ni kwa vile kinafanyika kwa uficho, badala ya kufanyika hadharani ili kila mtu ajue kile kianachoendelea, kwani kufanya hivyo kunaweza leta hatari ya kutolewa taarifa potofu.