Burundi kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi leo

0
581

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchini Burundi, leo inatarajiwa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais pamoja na Wabunge uliofanyika Jumatano iliyopita.

Matokeo hayo ya awali yanatarajiwa kutangazwa huku Evariste Ndayishimiye ambaye ni mgombea wa kiti cha Urais aliyeteuliwa na Rais wa sasa wa Burundi, – Pierre Nkurunziza akipewa nafasi kubwa ya kutangazwa mshindi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchini Burundi imeeleza kuwa matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu yatatangazwa Juni nne mwaka huu.

Matokeo yasiyo rasmi ya uchaguzi wa Rais nchini Burundi ambayo yamekuwa yakichapishwa na vyombo mbalimbali vya habari vya serikali ya nchi hiyo yanaonesha Ndayishimiye anaongoza kwa kupata asilimia 80 ya kura zote zilizopigwa.