Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amejiuzulu nafasi ya kiongozi wa Chama cha Conservative.
Boris amejiuzulu nafasi hiyo leo , lakini bado atabaki kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza mpaka chama hicho kitakapopata kiongozi mpya mwezi Septemba mwaka huu.
Katika hotuba yake, Boris amesema ana huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani na kwamba amekubali kuanza kwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya.
Boris amefikia uamuzi huo baada ya kuhudumu katika wadhifa huo tangu mwaka 2019.
Sababu kubwa ya kuachia wadhifa huo ni kundi kubwa la wanasiasa katika serikali yake kutokuwa na imani naye.