Bilionea Elon Musk anunua Twitter

0
249

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Tesla, Bilionea Elon Musk, amekamilisha mchakato wa kununua mtandao wa Twitter kwa dola bilioni 44 za Kimarekani.

Elon Musk amenunua mtandao huo baada ya miezi kadhaa ya mapambano ya kisheria.

Mpaka sasa mtandao huo wa Twitter haujatoa taarifa ya kuthibitisha jambo hilo, lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa suala hilo limekamilika.