Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, Joseph R. Biden Jr ameshinda kinyanganyiro cha urais nchini humo.
Biden amemshinda aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Donald Trump katika uchaguzi mkuu wa Marekani uliofanyika Jumanne kwa majimbo mengi ikiwemo jimbo la Pennsylvania lenye wawakillishi 20 na kufikisha zaidi ya kura 270.
Biden amepata kura 290 huku mpinzani wake mkubwa akipata kura 214 hadi sasa na kumfanya Biden kuwa Rais mteule wa 46 wa nchi hiyo.