Biden asema Putin hajui kinachokuja

0
214

Rais wa Marekani Joe Biden ameliambia Bunge la Marekani Kuwa Vladimir Putin alikosea mahesabu na hakujua jinsi nchi za magharibi zitakavyojibu baada ya uvamizi wake wa Ukraine

Kwenye hotuba yake kuu, Biden ameapa Kuwa demokrasia itashinda utawala wa kimabavu

Vyama vyote vya Democrats na Republicans viliungana kwa kusimama na kupiga makofi kuunga mkono msimamo huo.

Biden amesema Putin alidhani uvamizi huo ungewagawanya Wamerekani, na kusema Putin amekosea na Marekani ipo tayari.

Pia ametangaza kutoruhusiwa kwa ndege za Urusi kwenye anga la Marekani baada ya tangazo kama Hilo kwenye nchi za Canada na nchi za Ulaya.

Nchi ya Marekani na zile za umoja wa NATO wameshaweka vikwazo mbali mbali vya Kiuchumi na mifumo ya kifedha kwa Urusi na Putin mwenyewe .