Balozi Mchumo aula INBAR

0
353

Balozi Ali Mchumo ameteuliwa kuongoza Taasisi ya Kimataifa ya INBAR yenye makao yake Makuu nchini China.

Balozi Mchumo ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali, atahudumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitatu.

INBAR ni Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa yenye kushughulikia maendeleo endelevu ya mazingira kwa kutumia Mianzi (Bamboo) na Mhenzirani (Rattan).