Balozi Kombo awasilisha hati za utambulisho

0
284

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Malta, Dkt. George Vella.

Balozi Kombo amewasilisha hati hizo baada ya nchi zinazosimamiwa na ubalozi wa Italia kuongezeka, ambapo Malta ni moja ya nchi zinazosimamiwa na ubalozi huo.

Baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Vella, viongozi hao wawili wamefanya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tamzania Malta.