Aliyeua kwa risasi Thailand naye auawa

0
470

Polisi nchini Thailand wamesema kuwa askari aliyeua kwa risasi watu 26 katika mji wa Nakhon Ratchasima, naye ameuawa.

Askari huyo wa cheo cha chini Jakraphanth Thomma kabla ya kufanya mauaji ya watu hao alimshambulia kwa risasi na kumuua mkuu wa kambi na kuiba silaha kadhaa kambini hapo.

Mauaji hayo ya watu wengi aliyafanya kwenye mitaa ambako alikua akiwafyatulia risasi pamoja na katika eneo la maduka makubwa kwenye mji huo wa Nakhon Ratchasima.

Katika tukio hilo, watu wengine 57 wamejeruhiwa.

Kabla ya kufanya mashambulio hayo, katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Thomma aliweka picha ya bastola iliyo na seti tatu za risasi na kuandika maneno yanayosema “ni wakati wa kufurahi” na mengine yakisema “hakuna mtu anayeweza kuzuia kifo”.

Lakini mara tu baada ya kufanya mauaji hayo, katika ukurasa huohuo aliweka picha za matukio ya wakati alipokuwa akitekeleza shambulio hilo huku akiuliza kama inampasa kujisalimisha.