Aliyemng’oa Gaddafi madarakani afariki kwa Corona

0
1115

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa mpito nchini Libya, Mahmoud Jibril, amefariki dunia baada ya kupata maambukizi ya virusi vya Corona.

Imeelezwa kuwa kiongozi huyo wa zamani aliyeongoza mapinduzi yaliyomtoa madarakani marehemu Muammar Gaddafi mwaka 2011, alilazwa hospitali baada ya kupata mshtuko wa moyo na siku tatu baadaye, aligundulika kuwa na ugonjwa wa COVID-19 na kuwekwa karantini.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Ganzouri iliyopo mjini Cairo, Hisham Wagdy, amesema Jibril alifikishwa hospitalini hapo Machi 21, 2020, na alithibitishwa kuwa na virusi hivyo siku chache baadaye.

Ameeleza kuwa kiongozi huyo alikuwa akiendelea vizuri lakini hali yake ilibadilika ghafla na kusababisha kifo chake.