Aliyekutwa amefariki Marekani adaiwa ni Mtanzania

0
508

Wapelelezi nchini Marekani wamefanikiwa kuutambua mwili wa kijana aliyekutwa amefariki dunia kwenye fukwe huko Galveston sland, Texas miaka mitatu iliyopita.

Polisi wa Galveston wameutambua mwili huo kuwa ni wa Calvin Mbwambo (26), na kudai kuwa ni Mtanzania aliyekuwa masomoni nchini Marekani.

Mwili wa Calvin ulipatikana siku ya Mama Duniani mwaka 2020, lakini Wapelelezi hawakuweza kumtambua ni nani kwa kuwa hakuwa na utambulisho wowote.

Kwa kipindi chote hicho waliendelea kufanya uchunguzi wa
DNA na cha kwanza walibaini kuwa mwili huo haukuwa wa raia wa Marekani.

Pia walikagua nyaraka na rekodi za Serikali zinazowahusu Wanafunzi wa kigeni ambao hawajulikani walipo na alama za vidole zilionesha ni kweli mwili huo ulikuwa wa Calvin.

Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zinaeleza kuwa tayari polisi wa Galveston, Marekani wameitaarifu familia ya
Calvin
Mbwambo iliyopo Tanzania kuhusu kifo cha ndugu yao.

Chanzo cha kifo cha
Calvin bado hakijafahamika na taarifa za polisi zinaonesha hakuna dalili kuwa alifanyiwa ukatili wowote kabla ya kifo chake.

Mkasa wa kifo cha Calvin ulioneshwa hadi kwenye kipindi cha ABC13, Unsolved huko Marekani.