Bensalah Rais wa mpito Algeria

0
379

Abdelkader Bensalah ameteuliwa kuwa Rais wa mpito wa Algeria, kumrithi Abdelaziz Bouteflika  ambaye alijiuzulu kufuatia shinikizo la Jeshi la nchi hiyo pamoja na Raia wiki iliyopita, baada ya kukaa madarakani kwa kwa muda wa miaka Ishirini.

Bensalah ambaye ni Spika wa Bunge,  ataongoza Algeria katika kipindi cha mpito wakati uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo ukiandaliwa ndani ya kipindi cha siku Tisini.

Bensalah si mtu anayefahamika sana miongoni mwa Waandamanaji ambao wamekua wakiandamana kwa siku kadhaa,  kushinikiza kujiuzulu kwa Bouteflika.

Hata hivyo dakika chache baada ya kutolewa kwa tangazo la uteuzi wa Bensalah kuwa Rais wa Mpito, baadhi ya raia wa Algeria wamejitokeza katika mitaa mbalimbali ya nchi hiyo na kuandamana kwa lengo la kupinga uteuzi wake.