Alama 11 kutambua noti halali

0
1515
  1. Alama iliyofichika kwenye noti inayoonesha sura ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na thamani ya noti ya shilingi 10,000.
  2. Alama za vipande vipande zenye kuonesha thamani ya noti ya shilingi 10,000 inapomulikwa kwenye mwanga ambapo tarakimu kamili za thamani ya noti hutokea.
  3. Kivuli kilichofichika: Alama maalumu iliyofichika yenye kuonesha thamani ya noti ya shilingi elfu kumi huonekana kuwa angavu noti inapogeuzwageuzwa.
  4. Pembe zinazoparuza (nukta nundu) ni alama maalumu zinazotambulisha thamani ya noti kwa kuipapasa kwa wenye ulemavu wa macho.
  5. Alama maalumu ambayo Twiga anaonekana ndani yake, yenye rangi ya dhahabu ambayo hubadilika kuwa kijani na kurudia tena kuwa ya dhahabu noti inapogeuzwa.
  6. Maandishi madogo sana yaliyolala na kutuna yanayoonekana kwa kutumia vifaa maalum vya kukuzia maandishi.
  7. Nyuzi nyembamba zenye rangi tatu zilizofichika ambazo huonekana kwa kutumia mwanga maalumu wa rangi ya zambarau.
  8. Alama ya usalama iliyoboreshwa kwenye utepe mwembamba inaonesha kutembea na kubadilika kwa rangi. Rangi za utepe huo zinaonesha upinde wa mistari mithili ya mawimbi yanayotembea kutoka kushoto kwenda kulia na kinyume chake, pale noti hiyo inapogeuzwageuzwa upande au juu na chini. Rangi za utepe huo zinabadilika toka rangi ya pinki kwenda kijani.

Pia, unapoielekeza kwenye mwanga, kuna maneno yanayosomeka: ‘BOT 10000.’

  1. Alama ya wino maalumu uliofichika ambayo huangaza noti ikimulikwa kwa mwanga wa rangi ya zambarau.
  2. Namba ya noti yenye tarakimu ambazo zinazoongezeka ukubwa na kung’aa zinapomulikwa kwa mwanga maalumu wa rangi ya zambarau.
  3. Alama ya wino maalumu uliofichika ambao huonekana noti ikimulikwa kwa mwanga maalumu wa rangi ya zambarau.

Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania (BoT)