Anthony Hoyte amechora picha ya mtu mwenye sharubu kwa baiskeli ili kuhamasisha kampeni ya ‘Movember’ kwa kutumia programu ya mazoezi inayofuatiliwa na GPS, Strava.
Anthony Hoyte ameendesha baiskeli kwa umbali wa kilometa 121 na anatarajia kuchangisha Paundi 3925 (Milioni 12 za kitanzania) kwa ajili ya kampeni ya ‘Movember’.
Movember ni munganiko wa neno ‘Mo’ na ‘Vemba’ (kutoka Novemba) ambapo ni tukio la kila mwaka linalohusisha ukuzaji wa sharubu wakati wa mwezi wa Novemba ili kuongeza ufahamu wa masuala ya afya kwa wanaume. , kama vile saratani ya tezi dume na kujiua kwa wanaume. lengo la Movember ni kubadilisha muonekano wa afya ya wanaume.
Anthony Hoyte, ambaye alipata jina lake la utani la “Picasso” aliendesha baiskeli kwa saa nane na dakika 27 Jumamosi ili kuchora picha kwa kutumia programu ya kufuatilia njia ya mazoezi ya Strava.