Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 62 huko Magdeburg, Ujerumani anadaiwa kwa makusudi ama kwa sababu binafsi alipatiwa chanjo mara 217 dhidi ya Uviko ndani ya kipindi cha miezi 29.
Hata hivyo Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Erlangen – Nuremberg wamemfanyia vipimo mwanaume huyo ili kuona kama amepatwa na.madhara kutokana na kuchanjwa mara nyingi na kubaini kwamba hajapata madhara yoyote kutokana na kupatiwa chanjo mara zote hizo.
Katika taarifa yao waliyoichapisha kwenye jarida la The Lancet, Watafiti hao wamesema hakukuwa na dalili kwamba mwanaume huyo amewahi kuambukizwa Uviko.
Kwenye maeneo mengi duniani, chanjo dhidi ya Uviko imekuwa ikitolewa mara moja au mbili.