50 wanaswa kwenye vifusi baada ya jengo kuporomoka

0
259

Watu watano wamethibitika kufariki dunia baada ya jengo la ghorofa tano kuporomoka katika mji wa George nchini Afrika Kusini.

Habari kutoka nchini Afrika Kusini zinaeleza kuwa zaidi ya watu 20 wamejeruhiwa katika tukio hilo na wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini, huku kumi kati yao hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya.

Vikosi vya uokoaji nchini humo bado vinaendelea kuwatafuta watu wengine zaidi ya 50 wanaodaiwa kunaswa kwenye vifusi baada ya jengo hilo kuporomoka na tayari waokoaji wamewasiliana na baadhi ya watu walionaswa katika vifusi hivyo.

Zaidi ya wafanyakazi 100 wa uokoaji wakiwa na mbwa wa kunusa wako katika eneo hilo la tukio ili kujaribu kuokoa watu walionasa kwenye vifusi.

Wakati jengo hilo la ghorofa linaporomoka, kulikuwa na wafanyakazi 75 waliokuwa wakiendelea na kazi za ujenzi.