Vanesa Mdee azidi kupasua anga la kimataifa.

0
1250

Mwanamuziki na mwanaharakati wa haki za wanawake, Vanessa Mdee amefanikisha kurusha sehemu ya kwanza ya podcast yake ya ‘Deep Dive with Vanessa Mdee’ leo kwenye application ya Spotify, Google Podcasts na Apple Podcasts App.

Mdee ameweza kuzungumza juu ya msimamo wake juu ya haki za wanawake na nafasi za wakina mama katika jamii za kitanzania.

Zaidi, podcast hii itahusu maisha yake binafsi pamoja na mada mbalimbali zenye kuhamasisha.