Tyrese aimwagia sifa Zanzibar

0
322

Kupita ukurasa wake wa Instagram mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani, Tyrese Gibson amemwaga sifa za uzuri wa Zanzibar.

“Tafuteni kwenye google, hii sehemu ya kustaajabisha inaitwa ZANZIBAR, inapatikana sehemu ya Africa iitwayo TANZANIA, walituweka sote gizani kwa makusudi…. sisi huku Marekani HUWAONA WANYAMA TU KWENYE TV ZETU, hawataki hata mmoja wetu ajue utajiri na uzuri wa kweli wa AFRIKA.”

Tyrese ameigiza filamu nyingi na ambazo zimempatia umaarufu kama Fast and Furious na Black and Blue.