TUZO ZA AFRIMMA 2019

0
1810

Jumla ya majina 17 ya watanzania na Kundi moja la wacheza muziki wametajwa kuwania vipengele mbalimbali vya tuzo za AFRICAN MUZIK MAGAZINE AWARDS (AFRIMMA) 

AFRIMMA ni sherehe za tuzo za Diaspora ambazo zinaangazia aina zote za muziki ikiwa ni pamoja na: Afrobeats, Assiko, Bongo Fleva, Decale, Funana, Genge, Hiplife, Kwaito, Lingala na Soukous.

Mwaka huu waandaaji wa Tuzo za AFRIMMA nchini Marekani wametaja majina ya wanamuziki wanaowania Tuzo hizo. 

Msanii Diamond Platnumz kutoka Tanzania anaongoza kuwania vipengele 6, Ikiwemo  wimbo Bora wa mwaka , Msanii Bora wa mwaka  na Video Bora ya mwaka.

Vilevile Ommy Dimpoz pamoja na Alikiba  wote wametajwa kwenye vipengele vitatu tofauti 

Wasanii wengine ni Vanessa Mdee, Nandy, Rayvanny, Harmonize, Jux, Lil Ommy, S2Kizzy, Kimamba, Laizer, Dj D-Ommy, Director Kenny, H. Bajuni (Mchezaji wa Diamond Platnumz), Navy Kenzo (Aika na Nahreel) na kundi la kucheza la Rabit Crew 255.