Tuzo ya ubinafsi kwa TEMS

0
553

Mwanamuziki Temilade Openiyi maarufu
TEMS wa nchini Nigeria amelalamikiwa na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo za Oscars, baada ya kuvaa pambo kubwa kichwani lililowaziba wengine wasione yanayoendelea na hivyo kuzua gumzo mitandaoni.

Mwanamuziki huyo ameandika wimbo wa Rihanna wa Lift Me Up uliotumika kwenye filamu ya Black Panther na ambao Rihanna aliuimba usiku wa tuzo hizo.

Baadhi ya watu waliotoa maoni yao kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii wamemtunuku TERMS tuzo ya nguo ya kibinafsi zaidi kutokana na hatua yake ya kuvaa pambo hilo kubwa kichwani na kuwaziba wengine.

Tuzo za Oscars zimefanyika usiku wa kuamkia leo huko Carlifornia, Marekani.