TBC yatoa msaada wa matibabu kwa King Kiki

0
746

Msanii mkongwe nchini anayejulikana zaidi kwa wimbo wake wa ‘Kitambaa Cheupe,’ Kikumbi Mwanza, almaarufu King Kiki anapatiwa matibabu nyumbani kwake baada ya kufanyiwa upasuaji wa shingo.

King Kiki ambaye alifanyiwa upasuaji huo takribani miezi mitatu iliyopita kufuatia kusagika kwa zaidi ya pingili tano za uti wa mgongo, hali yake bado haijachachamaa kwani sasa anasumbuliwa na tatizo la ganzi mwili mzima.

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) chini ya Mkurugenzi Mkuu, Ayub Rioba Chacha tumemtembelea mwanamuziki huyo nyumbani kwake kumjulia hali na kumkabidhi kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya kumsaidia katika matibabu.

Constansia Kalanga ambaye ni mke wa mzee King Kiki amewasihi Watanzania na wapenzi wa muziki wa mumewe kumkumbuka kwa maombi bila kujali dini zao.

Aidha, amewaomba watakaoguswa kutoa msaada wa chochote kwa ajili ya kusaidia matibabu ya nguli huyo wa muziki Tanzania wanaweza kuwasiliana kupitia namba 0713311673.

Mbali na kitambaa cheupe, King Kikii ametamba na nyimbo mbalimbali ikiwa ni oamoja na mtoto kaanza tambaa, mtoto wa mjini na Coco.