Tanzana Safari Channel yawapeleka walimbwende hifadhi ya Taifa ya Nyerere

0
1897

Chaneli ya Utalii (Tanzania Safari Channel), kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya utalii imewapeleka washiriki wa shindano la urembo kwa kanda ya Mashariki (Miss Tanzania Eastern Zone), hifadhi ya Nyerere ambayo ni hifadhi kubwa zaidi Barani Afrika yenye eneo la kilometa za mraba 30,893.

Walimbwende wakiwa katika hifadhi ya Nyerere kutalii

Wakiwa katika hifadhi hiyo walimbwende hao wamepata nafasi ya kutalii wakati wa mchana na usiku, utalii wa boti ndani ya mto, utalii wa picha na utalii wa kitamaduni na historia.

Lengo la Utalii huu ni kuongeza umaarufu wa hifadhi ya Nyerere na kuchochea utalii wa ndani kwa kutumia hamasa ya shindano la urembo litakalofanyika tarehe 24/09/2021 mkoani Morogoro.