Mrembo Sylivia Sebatian Bebwa kutoka Kanda ya Ziwa, ameshinda taji la Miss Tanzania kwa mwaka 2019, katika shindano lililofanyika jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia hii leo.
Jumla ya Warembo Ishirini wameshiriki katika shindano hilo, ambapo mgeni rami alikua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe.
Kufuatia ushindi huo, Sylivia mwenye umri wa miaka 19, ameibuka na zawadi ya kitita cha Shilingi Milioni Kumi.
Sylivia ni Mhitimu wa Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Waja, na kwa sasa anasoma kozi ya Kompyuta.