Simba vs Ihefu kivumbi kwa Mkapa

0
1022

Simba SC inashuka dimbani hii leo kuwaalika walima mpunga wa Ubaruku Ihefu FC katika muendelezo wa Michezo ya Ligi kuu ya soka ya NBC msimu huu.

Simba inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi hiyo itamkosa kiungo wake raia wa Zambia Clatous Chama ambaye amefungiwa michezo mitatu, Peter Banda na Israel Mwenda ambao ni majeruhi.

Mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 1 jioni unatarajiwa kuwa na ushindani kwa kila upande.

Ihefu inaburuza mkia katika msimamo wa Ligi hiyo huku Simba ikiwa nafasi ya pili.

Mapema saa 10 jioni huko katika mashamba ya miwa Turiani, Mkoani Morogoro Mabingwa wa zamani wa Ligi hiyo Mtibwa Suger watawaalika wana rambaramba Azam FC katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.