Rapa DMX afariki dunia

0
282

Mwanamuziki wa mtindo wa Rap wa nchini Marekani, -Earl Simmons maarufu kama DMX amefariki dunia katika hospitali moja jijini New York akiwa na umri wa miaka 50.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa DMX ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo yuko katika uangalizi maalum kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha dawa za kulevya.

Hata hivyo kuna taarifa nyingine zinazosema kuwa, DMX amefariki dunia baada ya kupata shambulio la moyo.

DMX alianza kuimba muziki wa Rap mwanzoni mwa miaka ya 90 na albamu yake aliyoitoa mwaka 1998 ya It’s Dark and Hell Is Hot ilipata mafanikio makubwa baada ya kuuza zaidi ya kopi laki mbili na nusu katika wiki ya kwanza baada ya kuiachia.