Polisi wathibitisha kumtia nguvuni Msanii Diamond

0
2330
Msanii Nasib Abdul maarufu kama Diamond

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya DSM limethibitisha kumkamata Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul (Diamond) kwa kosa la kusambaza picha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa za kukamatwa kwa msanii huyo zilifahamika hii leo kwenye kikao cha bunge huko mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Katika Kipindi hicho Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema  msanii Diamond pamoja na Nandi watakamatwa na kupelekwa polisi kisha mahakamani kwa kuonyesha video zisizozingatia maadili ya kitanzania.