Nyota wa filamu ya Life of Pi, Irrfan Khan afariki dunia

0
1325

Irrfan Khan anajulikana kimataifa kwa uhusika wake katika Slumdog Millionea na Life of Pi, Khan alifanya kazi kubwa za filamu Bollywood nchini India ambazo ziliuza sana, ikiwa ni pamoja na Lunchbox, Piku na Medium Hindi.

Ametajwa kama “talanta ya kushangaza,” na Piku ambaye ni nyota mwenzake katika Amitabh Bachchan.

Wasimamizi wake katika kazi zake wanasema Khan amefariki katika hospitali iliopo mji wa Magharibi wa Mumbai ambapo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la utumbo mkubwa.

Khan aliyezaliwa Januari 7, 1967 amefariki akiwa na umri wa miaka 53.