Nyoshi El Saadat awahimiza vijana kushiriki Club Raha Leo Show

0
397
Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi Nyoshi El Saadat

Mwanamuziki wa muziki wa dance nchini Nyoshi El Saadat amewashauri vijana kuchangamkia fursa ya kuonyesha vipaji kupitia shindano la Club Raha Leo Show linaloendeshwa na TBC.

Akizungumza jijini Dar es salaam alipotembelea eneo la Coco Beach, kuangalia maendeleo ya usaili kwa ukanda wa mashariki Nyoshi amesema kujaribu ni njia ya kufikia malengo.

” Mimi mwenyewe kabla ya kufahamika nilifanya mazoezi sana na kujaribu fursa mbalimbali na kwa kufanya hivyo nilikuwa nikipata ushauri wa namna ya kufanya vyema zaidi hivyo vijana wasikate tamaa.” Amesema Nyoshi.

Shindano la kusaka vipaji vya kuimba na kucheza la Club Raha Leo show linaendelea kwa ngazi ya usaili wa awali Jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa usaili jijini Mbeya, Mwanza,Dodoma, na Arusha.

GODFRIEND MBUYA

MACHI 11,2018