Ndani hadi 2025

0
3225

Simba imefanikiwa kumbakisha kipa wake namba moja, Aishi Manula baada ya kukubali kusaini mkataba mpya utakaombakiza mtaa wa Msimbazi hadi mwaka 2025.

Manula amesaini mkataba huo wa miaka mitatu na Simba baada ya mkataba wake wa awali kumalizika.

Kipa huyo alijiunga na Simba mwaka 2017 akitokea Azam FC na akiwa Simba ametwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne, Kombe la Shirikisho hapa nchini mara mbili na ameifikisha Simba hatua ya robo ya ligi ya mabingwa barani Afrika mara mbili na mara moja hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.