Naomi Campbell ajikinga na corona

0
1266

Mwanamitindo, muigizaji na mfanyabiashara wa nchini Uingereza, -Naomi Campbell ameposti picha ya video katika mtandao wa kijamii wa Instagram inayomuonyesha akiwa amevalia vazi maalumu la kujikinga mwili mzima ( hazmat suit) ikiwa ni njia ya kujikinga na virusi vya corona.

Mara kwa mara Naomi amekua akivalia mavazi ya aina hiyo hasa wakati wa safari ili kujikinga na hatari mbalimbali, na katika video hiyo ya hivi karibuni ameonekana akiwa katika uwanja wa ndege wa Los Angeles nchini Marekani tayari kwa safari.

Vazi hilo (hazmat suit) mara nyingi limekua likitengenezwa kwa kutumia malighafi ngumu ama ya plastiki na limekua likihusisha kifaa cha kuziba mdomo, pua, macho na mikono (gloves).

Katika video hiyo, Naomi mwenye umri wa miaka 49 anaonekana pia akifuta maeneo yote yaliyo karibu na kiti alichokaa ili kuua vijidudu.

Virusi vya corona vilivyoanzia katika mji wa Wuhan nchini China, vimesambaa katika nchi mbalimbali duniani.