Nandy azindua Record Label

0
275

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva @OfficialNandy ametambulisha rasmi Record Label yake ‘The African Princess’, ambayo ameeleza lengo lake ni kuinua vipaji vya watoto wa kike tu.

“Ninayo furaha kubwa kuileta kwenu Rasmi THE AFRICAN PRINCESS LABEL…! 2023 label ambayo itahusisha wanawake tu!, kama tunavoona industry ya watoto wa kike ni chache sana na uthubutu umekuwa ni mdogo so tunaimani na kuomba the African princess label itaongeza wingi wa vipaji vya watoto wa kike waliopo mtaaani wenye ndoto kubwa ya kuwa wanamuziki!!.”

Nandy kwa sasa anawika na wimbo wa wake wa ‘Mchumba’.