Mtunzi na mwimbaji mkongwe wa nyimbo kutoka nchini Marekani John Prine amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 73.
Msemaji wa Prine amethibitisha kifo cha nyota huyo kwa niaba ya familia yake, ambapo ameeleza kuwa Prine John amefariki huko Vanderbilt baada ya kusumbuliwa na homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia, Prine alilazwa hospitalini mwezi uliopita baada ya kuonesha dalili za ugonjwa huo.
Mapema mwezi Machi mkewe alibainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, lakini alipona baada ya kupatiwa matibabu.