Mavunde: Dodoma tupo tayari na Serengeti Music Festival

0
413

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amesema Dodoma ipo tayari na wamejiandaa vyema kutoa ushirikiano wa kutosha katika Tamasha la Serengeti Music Festival litakalofanyika Februari 6, 2021 katika Uwanja wa Jamhuri.

Akizungumza na TBC ameishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kupeleka tamasha hilo mkoani humo na ametoa rai kwa vijana kutumia fursa za msimu wa tamasha, na fursa za sanaa kama ajira.

Wakati wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani wakisubiri kwa hamu tamasha hilo hapo kesho, usiku wa leo kutakuwa na ‘Pre-Party’ ambayo itarushwa mbashara kupitia Tanzania Safari Channel kuanzia saa 3 usiku.

Kwenye king’amuzi cha Azam ni chaneli namba 401, DSTV ni 292, Zuku ni 27, Startimes ni 331. Pia, unaweza kutufuatilia kupitia ukurasa wa YouTube kwa jina la Tanzania Safari Channel. Usikubali kupitwa na uhondo huu.