Marekani yashinda taji la ‘Miss Universe’

0
345

Mrembo R’bonney Gabriel kutoka Marekani Kaskazini ameshinda taji la ulimbwende la  ‘Miss Universe’ wa 71 ambapo zaidi ya walimbwende 80 kutoka duniani kote walichuana kuwania taji hilo.

Mshindi wa ‘Miss Universe’ R’Bonney Gabriel ana umri wa miaka 28, ni mbunifu wa mitindo, mwanamitindo na mwalimu kutoka Houston, Texas na ni Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Kifilipino kushinda taji la Miss USA.