Mambo yaliyozingatiwa kuchagua vazi la Taifa

0
350

Kamati inayoshughulikia mchakato wa upatikanaji wa vazi la Taifa imeongezea wazo la kamati iliyopita la kupatikana kwa kitambaa na kutaka kuwepo pia kwa mshono wa Taifa ili kuongeza wigo mpana wa machaguzi ya wananchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Vazi la Taifa Profesa Hermas Mwansoko amesema kamati yake imependekeza kuwepo pia kwa michoro ya utambulisho wa tunu na nembo mbalimbali za Taifa ikiwemo, Tembo, Tanzanite, mlima Kilimanjaro, Nembo ya Taifa, rangi za Bendera na alama za kuonyesha Muungano.

Profesa Mwansoko amesema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla iliyoandaliwa na wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa lengo la kutoa taarifa ya mchakato wa Vazi na Mdundo wa Taifa na awamu ya pili ya utoaji mkopo kwa wasanii.