Takribani watu elfu 20 walikusanyika kusherehekea maisha na urithi wa Takeoff wakati wa ibada ya ukumbusho wake huko Atlanta. Wasanii mbalimbali walihudhuria hafla hiyo akiwemo Offset, Quavo, na Drake, pamoja na Justin Bieber, Chloe Bailey, na Yolanda Adams.
Msanii Kirsniki Khari Ball maarufu Takeoff ni raia wa Marekani, mwanamuziki katika kundi la Migos ambaye siku chache zilizopita alipigwa risasi na akiwa anacheza mchezo wa kete jijini Houston na kufariki papo hapo.
Takeoff alikuwa mwanamuziki mdogo zaidi kwa umri katika kundi la Migos ambalo liliundwa mwaka 2008 huko Georgia nakuachia ngoma yao ya kwanza iliyokwenda kwa jina la “Versace” mwaka 2013.
Hata hivyo siku chache kabla ya kifo chake kundi hilo liliachia ngoma mpya yenye jina la “Messy” ambayo inaonekana ikifanya vizuri kwa kutazamwa kwenye mtandao wa YouTube na mamilioni ya watu ndani ya siku chache.