Lil Wayne abaini nchi ya asili yake ya Afrika

0
1211

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Dwayne Michael Carter Jr maarufu kama Lil Wayne amesema kuwa uchunguzi wa kihistoria umeonesha kuwa asili yake ni nchini Nigeria kwa asilimia 53.

Rapa huyo amesema hilo katika mahojiano na kituo cha runinga cha Revolt (TV), na amebainisha kwamba ana mpango wa kutembelea taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mwenyekiti wa Wanaigeria wanaoishi nje ya nchi, Abike Dabiri amesema kuwa anatazamia kumkaribisha Wayne nchini Nigeria.

Kupitia mitandao ya kijamii baadhi ya raia wa Nigeria wamefurahishwa na kauli hiyo na kumkaribisha nchini humo, lakini wengine wameshtushwa na wimbi la watu mashuhuri kutoka Marekani kuonesha kuwa na uhusiano wa kiasili na baadhi ya nchi za Afrika.