Kocha Nabi alalamikia ratiba ya ligi

0
1033

Kocha mkuu wa Mabingwa wa Tanzania, Yanga SC, Nasredeen Mohamed Nabi amelalamikia ratiba ya Ligi kuu ambayo amesema haitoi nafasi kwa wachezaji wake kupata muda wa mapumziko.

Yanga imecheza michezo ya ligi kuu na mechi za mtoano za Kombe la Shirikisho barani Afrika matawalia na wamerejea jana, na kesho Jumapili wanapaswa kucheza na Kagera Sugar.

Akizungumza za waandishi wa habari jijini Mwanza kocha Nabi amesema tangu wacheze siku ya Jumatano na Club Africain hawajapata muda wa kufanya mazoezi na kesho wanapaswa kucheza dhidi ya Kagera.

Licha ya ugumu huo wa ratiba, Nabi amewataka wachezaji wake kupambana na kushinda mchezo huo.

Kwa upande wake kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema wapenzi wa soka watarajie burudani safi kutoka kwa vijana wake katika mchezo huo.