Khosi aondoka na milioni 200

0
529

Mwanadada Khosi Twala (25) kutoka Afrika Kusini ameibuka mshindi wa shindano la Big Brother Titans lililojumuisha washindani 24 kutoka Afrika Kusini na Nigeria.

Mshindi huyo mbali na mali nyingine ziambatanazo na ushindi huo, ikiwemo nyumba, amejishindia dola 100,000 za kimarekani sawa na shilingi milioni 233 za Kitanzania.

Hadi kufikia fainali Khosi alikuwa akichuana na Kanaga Jnr ambaye amekuwa mshindi wa pili.

Kwa hapa nyumbani, Richard Bezuidenhout na Idris Sultan waliwahi kushinda mashindano ya Big Brother Afrika kabla ya kufutwa na kuundwa Big Brother Titans na Big Brother Naija.