JINSI YA KUPAMBA MEZA

0
364

Meza yako inabadilisha mwonekano wa sebule yako kutegemea na utakavyoipamba kuna muda unaweza kuiacha bila pambo lolote lakini muda ambao unataka nyumba yako iwe pambe na kuvutia kwa kutumia nakshi zifuatazo:

MAUA: Unaweza kutumia maua ya asili au bandia itategemea na chaguo lako wewe, maua yako sio lazima yawe na rangi inayoendana na vitu nyumbani kwako yanaweza kuwa na rangi tulivu ambazo zipo rafiki na kwa kila pambo. Maua yako unaweka kwenye chombo maalumu “vessels” ambayo ikosambamba na ukubwa wa maua na aina ya maua yenyewe

MISHUMAA: Mishumaa huleta mwanga lakini pia mvuto wa kupendezesha meza yako mara nyingi mishumaa ina nakshi yake ya pekee unaweza weka mishumaa mikubwa au midogo kutegemea na tray au ukubwa wa meza yako

VITABU NA MAJARIDA: Kuna muda kitabu kinageuka pambo baada ya kukuelimisha au mfano wa boksi la kitabu ambalo unaweza kununua katika maduka ya mapambo
Unaweza kuweka kitabu mezani kwa usawa wa pambo lingine kama maua na ikawapambe….!!!

SINIA (TRAY) : Sinia la kupambia linaweza kuwa la mbao au la chuma ukubwa unategemea na meza yako na mapambo unayotaka kuweka kwenye meza yako mfano mishumaa ,maua au mapambo mbalimbali

VESSELS: Haya ni mapambo ya kisasa na kitamaduni mara nyingi ni mfano wa chupa au kombe kubwa lenye muundo wa tofauti tofauti ambayo hivi sasa unaweza kupata kwenye maduka ya mapambo na meza yako ikadamsh na kupendeza